Walinda amani wa UNIFIL nchini Lebanon wasimilia kinachowakabili mashambulizi ya Israel yakiendelea
MP3•Episoder hjem
Manage episode 447277564 series 2027789
Innhold levert av UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations. Alt podcastinnhold, inkludert episoder, grafikk og podcastbeskrivelser, lastes opp og leveres direkte av UN Global Communications (Digital Solutions Unit) and United Nations eller deres podcastplattformpartner. Hvis du tror at noen bruker det opphavsrettsbeskyttede verket ditt uten din tillatelse, kan du følge prosessen skissert her https://no.player.fm/legal.
Kikosi cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, ambapo, katikati ya mvutano unaoongezeka kati ya Lebanon na Israel, walinda amani walioko katika makao makuu ya UNIFIL huko Naqoura wamekuwa wakivumilia mazingira magumu. Ushuhuda wa hivi karibuni kutoka kwa walinda amani hao unaonesha ukubwa wa changamoto wanazokabiliana nazo, ikiwemo vitisho vilivyoongezeka kutoka kwa shughuli za kijeshi za Israel zilizo karibu na eneo hilo, vizuizi vya kusafiri, na changamoto za uendeshaji wa shughuli. Kupitia video ya Kikosi hicho cha muda cha Umoja wa Mataifa nchini Lebanon, UNIFIL, tunaona picha ya makao makuu yake huko Naqoura, Lebanon. Hapa tunaona ofisi za walinda amani hao, karibu na ofisi hii kuna mnara wa ulinzi, sehemu yake ikiwa imeharibiwa na mlipuko. Meja Kalpani Fernando anaelekeza kwenye mnara huo akieleza kilichotokea.“Ghafla, tuliona, na kusikia mlipuko. Kisha tukaona vumbi kubwa likitokea na moshi mweusi. Tulikimbia ndani ya ofisi, na ndani ya sekunde chache, mlipuko wa pili ulitokea. Kisha wanajeshi wawili kati ya kikosi changu walijeruhiwa walipokuwa wakifanya kazi katika Kituo cha Uangalizi cha 6. Walikuwa nje ya Kituo cha Uangalizi wakati huo, na walijeruhiwa kutokana na mlipuko wakati huo. Kisha nikafunga lango, na tukawapeleka hospitalini ndani ya muda wa dakika mbili hadi tatu.”Ingawa mzozo huu umesababisha madhara kwa afya ya walinda amani hawa, huku baadhi yao wakipata upasuaji kutokana na majeraha, bado wanaendelea kuwa na dhamira ya kuhudumu katika ujumbe wa kulinda amani. Mmoja wao ni Koplo Wickramage akisema….‘‘Wakati nilipokuwa kwenye zamu katika Kituo cha Uangalizi cha 6, kulitokea mlipuko na nikajeruhiwa kwenye sehemu ya nyuma ya bega langu. Nilihamishwa haraka kwenye hospitali ya UNIFIL. Nimefanyiwa upasuaji, na ninaendelea na matibabu. Sasa, ninapata nafuu na natumai kuungana na walinda amani wa Sri Lanka hivi karibuni ili kurudi kuhudumu katika UNIFIL.”Mbali na majukumu yao ya kawaida, wafanyakazi wa afya wa UNIFIL wamekuwa wakifanya kazi kwa bidii, wakitoa huduma si tu kwa walinda amani waliojeruhiwa bali pia kwa raia walionaswa katikati mwa mapigano hao kama anayoeleza Luteni Kanali Shilpi Mankotia,“Mbali na huduma za kawaida za matibabu, siku hizi tunatoa msaada na huduma kwa majeruhi na manusura waliolengwa kimakosa, ikiwa ni pamoja na raia na wahudumu wa kibinadamu. Nilikuwa kwenye likizo niliposikia kuhusu mzozo unaoendelea kwa sasa. Nilirudi kazini mara moja kutoka India. Nilifika Beirut usiku wa manane na baada ya kupambana kwa siku saba, hatimaye niliweza kurudi kwenye kituo changu cha kazi.”
…
continue reading
101 episoder