Artwork

Innhold levert av Iran.Tanzania. Alt podcastinnhold, inkludert episoder, grafikk og podcastbeskrivelser, lastes opp og leveres direkte av Iran.Tanzania eller deres podcastplattformpartner. Hvis du tror at noen bruker det opphavsrettsbeskyttede verket ditt uten din tillatelse, kan du følge prosessen skissert her https://no.player.fm/legal.
Player FM - Podcast-app
Gå frakoblet med Player FM -appen!

ATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI

7:16
 
Del
 
Manage episode 337502592 series 3382153
Innhold levert av Iran.Tanzania. Alt podcastinnhold, inkludert episoder, grafikk og podcastbeskrivelser, lastes opp og leveres direkte av Iran.Tanzania eller deres podcastplattformpartner. Hvis du tror at noen bruker det opphavsrettsbeskyttede verket ditt uten din tillatelse, kan du følge prosessen skissert her https://no.player.fm/legal.

ATTAR NEYSHABURI MALENGA WA KIIRANI

Tarehe 25 Farvardin kwa mujibu wa ( Kalenda ya Kiirani) inayosadifiana na tarehe 14 Aprili, ni siku ya kumkumbuka na kumuadhimisha malenga wa Kiirani Farid al-Din Abu Hamid Muhammad bin Abu Bakr Ibrahim bin Is- haq Attar Neyshabouri, ambaye ni mmoja wa washairi mashuhuri, aaref na mwanafikra mkubwa wa Kiirani aliyeishi mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa karne ya saba Hijria. Baadhi ya wanahistoria wameandika kuwa, mwanafikra na malenga huyo wa Kiajemi amezaliwa mwaka 513 na wengine wanaeleza kuwa alizaliwa mwaka 537 Hijiria.

Attar Neyshabouri alizaliwa katika kijiji cha Kadkan au Shadiakh, ambacho wakati huo kilikuwa sehemu ya jiji la Neyshabour. Hakuna habari inayoelezea taarifa zake za utotoni mwake, isipokuwa baba yake aliishi katika mji wa Shadiakh akifanya kazi ya kuuza dawa za asili, na alikuwa mahiri na hodari mno katika biashara hii ya kuuza dawa za asili, na baada ya kufariki dunia baba yake, Farid al Din Attar Neyshabouri aliendeleza shughuli za marehemu baba yake ya kuuza dawa za asili. Wakati akishughulika na uuzaji wa dawa za asili Attar Neyshabouri alikuwa akitoa tiba ya asili na wala haijulikani utaalamu huo wa kutoa tiba ya asilii aliupata kutoka kwa nani. Attar Neyshabouri aliendelea na shughuli zake za kutoa tiba ya asili sanjari na kuuza dawa za asili hadi pale yalipopatikana mapinduzi ya kiroho na kimaanawi kwa upande wake, na jambo hili limebainishwa kwa kutolewa visa kadhaa, lakini kisa maarufu ni hiki kifuatacho:

“Siku moja Attar Neyshabouri alikuwa dukani kwake akifanya shughuli zake, mara akaingia “Darwesh" na akaanza kusema maneno kadhaa yanayohusiana na Mwenyezi Mungu, ili Attar aweze kuvutika na kumsaidia, lakini Darwesh hakupata msaada wowote kutoka kwa Attar Neyshabouri. Darwesh akamwambia Attar : Ewe kijana unataka ufariki duniani kwa kifo cha namna gani? Attar akajibu: Kwa njia ileile ambayo wewe unataka kufa. Darwesh akasema; Wewe unataka kufa kama nitakavyokufa mimi? Attar akajibu: Ndio, Darwesh akachukua bakuli lake lililotengenezwa kwa mbao na kuliweka chini ya kichwa chake na akasema maneno ya Mwenyezi Mungu na hatimaye kufariki dunia. Kwa vile Attar Neyshabouri aliliona tukio hilo kwa macho yake aliathirika mno na kubadilika na akaamua kutoka dukani na kubadilisha kikamilifu mtindo na mwenendo wa maisha yake” .

Attar Neyshabouri aliposhuhudia tukio hilo la Darwesh , akaacha kabisa shughuli za tiba na biashara za dawa za asili, na akaamua kuelekea kwa Sheikh Mkuu Aref Rukniddin Akaf , wakati huo Sheikh Aref alikuwa mtu maarufu na mashuhuri mno na kwa miaka kadhaa Attar Neyshabouri alikuwa akipata elimu na maarifa kutoka kwa sheikh Aref Rukniddin Akaf.

Attaf Neyshabouri aliweza kutumia nusu ya umri wake kwa kufanya safari katika miji mbalimbali, na katika safari zake hizo alifanikiwa kukutana na masheikh wakubwa wakubwa katika zama hizo, na safari hizo ziliweza kumfikisha hadi kwa sheikh Majiduddin Baghdadi.

Inasemekana kuwa Sheikh Aref alipofikia marika ya uzee, Bahauddin Muhammad baba wa Jalaluddin Balkhi alikuwa pamoja na mwanawe walifanya safari ya kuelekea Iraq , wakiwa njiani walipitia Neyshabouri na wakafanikiwa kumtembelea Attar Neyshabouri, hivyo Sheikh Attar Neyshabouri alitoa nakala moja kati ya makala zake za mashairi na kumpa Jalaluddin ambapo wakati huo alikuwa bado kijana mdogo mno.

--- Send in a voice message: https://podcasters.spotify.com/pod/show/irantanzania/message

  continue reading

12 episoder

Artwork
iconDel
 
Todos os episódios

×
 
Loading …

Velkommen til Player FM!

Player FM scanner netter for høykvalitets podcaster som du kan nyte nå. Det er den beste podcastappen og fungerer på Android, iPhone og internett. Registrer deg for å synkronisere abonnement på flere enheter.

Hurtigreferanseguide

Copyright 2024 | Sitemap | Personvern | Vilkår for bruk | | opphavsrett